Sunday, 15 September 2013

KATIBA YA KIKUNDI



     


 KATIBA YA MAKUMBUSHO YOUTH DEVELOPMENT GROUP   
                                      (M.Y.D.G)
1. LENGO LA M.Y.D.G
Kwa hiari yetu wenyewe bila kulazimishwa na mtu sisi vijana wa makumbusho tumeamua kuanzisha kikundi hiki malengo yakiwa ni;
a) Nikufahamiana,kusaidiana,na kushirikiana katika  maisha yetu ya kila siku.
b) Kutembeleana,kujuliana hali  katika shida na raha kama kufiwa,harusi,kuuguliwa na sherehe
     mbalimbali.
c) Kuinua na kustawisha hali ya uchumi  na maisha ya mwanachama kwa njia ya ushauri na pesa
2. SIFA ZA MWANA M.Y.D.G
a)      Ajue kusoma na kuandika
b)     Awe na umri wa miaka 18 na kuendelea na awe raia wa Tanzania
c)      Awe na nidhamu ya M.Y.D.G
d)     Awe tayari kutoa michango yote ya chama na kutii masharti ya M.Y.D.G
e)      Awe na akili timamu
f)       Awe na moyo wa kujitolea na mwaminifu
g)      Awe anatokea makumbusho na maeneo ya karibu
3. WAJIBU WA MWANA M.Y.D.G
a)      Kuhudhuria mikutano yote ya M.Y.D.G
b)     Kulipa ada ya kila mwezi na kwa wakati unaotakiwa
c)      Kulipa michango ya sherehe,Msiba,kwa mda unaotakiwa
d)     Kutoa michango ya mawazo katika M.Y.D.G.
e)      Kushiriki katika matukio yanayowahusu wana M.Y.D.G katika  msiba na sherehe
4. MICHANGO YA M.Y.D.G
a) Kiingilio ni shilingi 3000/=(Elfu tatu)
b) Ada ya mwanaM.Y.D.G kwa mwezi ni shilingi 2000/=(Elfu mbili)
c) Kuchangiana kwa wana M.Y.D.G ni kama ifuatavyo
        i.            Kuoa/kuolewa mwana M.Y.D.G -20000/=(Elfu ishirini)
      ii.            Kupata mtoto -1000/=(Elfu moja)
    iii.            Misiba -3000/=(Elfu tatu)
    iv.            Mwana M.Y.D.G akifa 10000/=(Elfu kumi)
      v.            Kuumwa 10000/=(Elfu kumi)
NB:Mwana M.Y.D.G  akifa au akifiwa  kamati itajadili na chama kitatoa /kuchangia 25000/=(Elfu ishirini na tano) pia mwana M.Y.D.G unashauriwa kutoa taarifa mapema kwenye uongozi husika ili kuweza kujipanga mapema kumsaidia.
5. MAJUKUMU NA KUSAIDIANA KATIKA M.Y.D.G
Mwana M.Y.D.G  akiumwa au kuuguliwa yafutayo yafanyike
a)      Atembelewe na wana M.Y.D.G
b)     Kusaidiwa  na kuchangiwa  ikiwa ugonjwa ni mkubwa endapo ikafikiaakashindwa kufanya shughulizake za kila siku
c)      Kusaidiana kimaisha kwa kila mwana M.YD.G mfano kusaidiana mawazo ya kukabiliana na changamoto za kimaisha,kibiashara na kimaendeleo
6. MIIKO YA M.Y.D.G (SHERIA NA TARATIBU ZA KUFUATA)
a)      Kutotoa taarifa za uongo kwa wana M.Y.D.G au uongozi kwa kutaka kujinufaisha
b)     Fitina,majungu havina nafasi  ndani ya M.Y.D.G.
c)      Kuiba,kupoteza au kuharibu mali ya M.Y.D.G
d)     Kwenda kinyume na katiba ya M.Y.D.G.
e)      Kutotoa siri za M.Y.D.G.
f)       Kila mwanakikundi anatakiwa kuhudhuria  vikao vyote vya M.Y.D.G
NB:Mwana M.Y.D.G akivunja sheria adhabu kali itatolewa  ikiwemo kufukuzwa au kupigwa faini
7. KUTOHUDHURIA VIKAO VYA  M.Y.D.G
a)      Mwana M.Y.D.G  asipohudhuria kikao bila taarifa  atalipa faini 1000/=
b)     Mwana M.Y.D.G akichelewa kufika kwenye kikao bila taarifa  atatozwa faini 500/=
c)      Mwana M.Y.D.G asipohudhuria  vikao vitatu (3) mfululizo bila taarifa atakuwa amejitoa katika M.Y.D.G na Hatolipwa chochote
d)     Kikao kitafanyika mara moja kwa mwezi
8. KUTOLIPA MICHANGO YA M.Y.D.G
a)      Mwana M.Y.D.G asipolipa michango zaidi ya miezi mitatu atakuwa amejitoa kwenye M.Y.D.G.
b)     Mwana M.Y.D.G atakayeshindwa kulipa michango mingine kama vile sherehe atalipa faini ya 1000/= zaidi.
c)      Ni wajibu wa kila mwana M.YD.G  kuchangia kila michango ili kusudio letu la kusaidiana kwenye shida na raha litimie.
d)     KUKABIDHI PESA ZA MISIBA NA SHEREHE
                                 i.            Mwana M.Y.D.G akifiwa au akiwa na sherehe siku ya kumkabidhiwa fedha zake ikiwa anadaiwa madeni yote yatakatwa ndipo atakabidhiwa pesa yake iliyobaki.


9. UONGOZI WA M.Y.D.G
Ø  Mwenyekiti na makamu wake - 2
Ø  Katibu na makamu wake           -2
Ø  Mweka hazina                             -1
Ø  Afisa Habari wa M.Y.D.G           -1
Ø  Wajumbe wa kamati kuu
                    i.            Mwenyekiti/Makamu mwenyekiti
                  ii.            Katibu/Makamu
                iii.            Mweka hazina
                iv.            Wajumbe watakaochaguliwa
10. KAZI ZA VIONGOZI WA M.Y.D.G
        i.            KAZI  YA MWENYEKITI
Ø  Kuongoza  vikao vya M.Y.D.G na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa maamuzi ya M.Y.D.G
Ø  Atakuwa msemaji mkuu wa M.Y.D.G
Ø  Atakua ni mtetezi  na misimamizi wa  maamuzi na katiba ya M.Y.D.G
Ø  Kuweka saini nakuidhinisha matumizi ya M.Y.D.G.
      ii.            KAZI ZA  KATIBU
Ø  Atakuwa  mtendaji mkuu wa M.Y.D.G.
Ø  Kuandika na kutunza kumbukumbu za M.Y.D.G.
Ø  Atakuwa mshauri wa M.Y.D.G.
Ø  Ataitisha vikao vyote  vinavyohusu  mfuko wa kikundi baada ya kushauriana na mwenyekiti

    iii.            KAZI ZA  MWEKA HAZINA
Ø  Atawajibika  kupokea na kutunza taarifa  za mapato na matumizi  ya M.Y.D.G.
Ø  Kupokea  michango  ya M.Y.D.G  na kutunza  kumbukumbu za fedha katika M.Y.D.G.
Ø  Kutoa taarifa za mapato na matumizi ya fedha za M.Y.D.G kila mwezi

    iv.            KAZI ZA WAJUMBE
Ø  Kuhudhuria vikao vya kamati ya utendaji
Ø  Kutetea na kusimamia maslahi ya M.Y.D.G.
Ø  Kuchangia michango yote ya chama  na wana M.Y.D.G.





11. KUJITOA AU KUTOLEWA UANACHAMA
a)      Mwanachama atatoa notisi  ya miezi mitatu(3) kabla ya kuacha uanachama
b)     Uanachama utakoma  pale tu mwanachama anapofariki na chama kitatoa pesa shilingi 25000/=(elfu ishirini na tano) kama rambi rambi.
c)      Aidha uanachama utakoma pale mwanachama  anaposhindwa kutekeleza  sehemu ya ( ) ya katiba hii
d)     Kabla ya kutolewa uanachama mwanachama ataonywa  kwanza
e)      KAMA MWANACHAMA  ANJITOA KWASABABU ZA MSINGI MFANO
·         KUHAMA KUTOKA TANZANIA KWENDA NJE YA NCHI
i) CHAMA KITAMPA MKONO WA KWA HERI ROBO YA MICHANGO YAKE   
    YOTE
ii) NAKUPEWA GAWIO NI MPAKA KAMATI KUU IPITIE MAOMBI YAKE NA   
    WAJUMBE KURIDHIA
12. MUDA WA VIONGOZI MADARAKANI
a.      Viongozi watachaguliwa kila baada ya mwaka mmoja (1)
b.      Uongozi uliopo madarakani unaweza  kuendelea ikiwa huduma yao imekubalika na wana M.Y.D.G.
c.       Kiongozi anaweza  kuachishwa uongozi muda wowote ikiwa ataonekana  hafai kwa sababu za msingi  kwa mfano,
·         Kuvunja katiba ya M.Y.D.G.
·         Utovu wa nidhamu
·         Kutumia madaraka vibaya
·         Kutumia jina la kikundi kwa manufaa yake
·         Kiburi na jeuri
13. UCHAGUZI WA VIONGOZI
a)      Kikao cha uchaguzi ili kupitisha uchaguzi ufanyike lazima  kuwe na wajumbe ambao idadi yao haigawanyiki kwa 2
b)     Uchaguzi utafanyika  endapo tu kuna nusu ya wanachama wote
c)      Uchaguzi utakuwa unafanyika kila baada ya mwaka mmoja wa uongozi
14. SIFA ZA KIONGOZI
a)      Awe na umri kuanzia miaka 18
b)     Awe ni mzaliwa wa Tanzania
c)      Ajue kusoma na kuandika kwa ufasaha
d)     Awe mwenye nidhamu na kuijua vizuri katiba ya M.Y.D.G

15. KUFA KWA M.Y.D.G
M.Y.D.G kinaweza kufa kutokana na sababu zifuatazo
a)      Kufutwa na mamlaka yoyote halali ya serikali na sababu za halali za kisheria mfano.
·         Udini
·         Siasa
·         Ukabila
b)     Endapo umoja utakufa  utaacha kazi zake mali zake zote zinazohamishika na zisizohamishika kwa usimamizi wa Baraza la wajumbe la umoja zitapigwa mnada na fedha zote zitatumika kulipa madeni ya umoja kama yapo,
NB:Kama mwana M.Y.D.G atajihusisha na yaliyotajwa hapo juu hatua kali zitachukuliwa dhidi yake,ikiwa ni pamoja  na kusimamishwa uanachama kwa mujibu wa katiba hii.
16. MAPATO NA MATUMIZI
a)      Kila baada ya miezi mitatu lazima uongozi utoe na kuelezea kwa maandishi mapato na matumizi kwa wanachama wote,mweka hazina atasoma mapato na matumizi.
b)     Kila mwanachama anatakiwa kupewa risiti yake ya kila malipo na michango
17. VYANZO VYA MAPATO
     a)  Ada za wanakikundi kila mwezi
     b) Adhabu kwa wachelewaji(faini)
18. AKAUNTI YA BENKI YA M.Y.D.G
M.Y.D.G kitakuwa na akaunti namba ………. itakayomilikiwa na M.Y.D.G, pia itakuwa ni akaunti moja ambayo wanachama watakuwa wamechagua kwa kutunzia pesa za M.Y.D.G.Na uchukuaji wa pesa utahusisha watu wasiozidi wanne(4) wakiwemo mwenyekiti, katibu, mweka hazina na mjumbe mmoja.
19. MAREKEBISHO YA KATIBA
Katiba itafanyiwa marekebisho pale itakapoonekana ina mapungufu,na mapendekezo ya wajumbe ndiyo yatakayopelekea kufanyiwa marekebisho.Marekebisho yatafanyika kama nusu ya idadi ya wajumbe waliopendekeza hayo watakuwa /watakuepo kwenye kikao hicho.
NB: MWANA M.YDG ATAKAYEBAINIKA NA UBADHIRIFU WA MALI YA M.Y.D.G ATASHTAKIWA KWA SHERIA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

                      MUNGU BARIKI MAKUMBUSHO YOUTH DEVELOPMENT GROUP.

1 comment:

  1. Teton D.O.T. and Teton D.O.T. are made by grinding
    Teton D.O.T. is made by grinding anodized gold citizen eco drive titanium watch for use in the is titanium a metal dried titanium pry bar foods, and titanium dioxide skincare with this recipe ford transit connect titanium the habanero is a staple of all natural $4.75

    ReplyDelete